Ukiona Hivyo ujue Moyo Wake Na Hisia Zake Za Mapenzi Zimepungua Juu Yako Na Hana Furaha Tena Na Wewe Na Bado Kidogo Ataondoka.

Utake usitake jambo halitokei bila dalili, hata mvua haitokei ikanyesha tu bila mawingu kuonekana. Hata kama sie mwanaume mwingine ndo anamchanganya ila dalili hizi zinaonyesha inawezekana mwisho wa uhusiano ndo kitu kikubwa kinachofatia, na wala usiwaze ndoa.

"Hata ukifumba macho, ukitaka kuudanganya moyo kwamba kila kitu kiko sawa!, Kasoro lazima ionekane, jinsi anavyo fanya mambo sio tena kama siku za mwanzo alivyokua, hisia nawe hana tena, hizi ndizo dalili, ukiziona, neno moja tu linalofatia... Jipange!''

Utake usitake jambo halitokei bila dalili, hata mvua haitokei ikanyesha tu bila mawingu kuonekana, hata kama sie mwanaume mwingine ndo anamchanganya ila dalili hizi zinaonyesha inawezekana mwisho wa uhusiano ndo kitu kikubwa kinachofatia, na wala usiwaze ndoa..
  • Anaanza kukuona unamapungufu kwa kila unachofanya....
Msichana alie na furaha kwenye uhusiano hata kidogo hawezi kuona kasoro ndogo ndogo ulizonazo, hata uwe mnywaji atalewa na wewe, uwe mkacha vipindi darasani... atatoroka na wewe!, ila mapungufu kwenye uhusiano yakishaingia utaona kama yupo mkali wakati wote, kila ufanyacho kwake kibaya... tisheti uliovaa leo ni chafu wakati siku zote alikua anaiona inang'aa kama theluji.
  • Yupo bize kila wakati....
Zamani ilikua ukimpigia simu muonane hata kama ni saa tisa usiku, atapata nafasi kujakukusikiliza, hata kama usingizi umejaa usoni yupo radhi kukiacha kitanda aje akusikie tu ukitamka maneno yako matamu... ila sasa kila miadi unayotoa... jibu ni moja tu NIPO BIZE... Ntatafuta mda badae ntakuja nikuone!, baadae yenyewe sasa uliyoambiwa... subili milenia ijayo!.
  • Hakuambii tena saa ngapi ana muda muonane.... 
Yale ya zamani ya ''Honey mie kesho nipo free fanya basi tuonane!'', hayapo tena fanya kusahau. Hana mda tena na wewe, imekua wewe ndo unaepanga miadi, yeye wala... hana hata wazo wewe upo mjini!, hata ile hamu aliyokua nayo na wewe imeshapotea..., hata kufanya vitu vinavyokuonyesha hata kuna ukaribu kidogo na wewe hamna, ukiona hivi kaka jipange!.
  • Hakupigii tena simu, wewe ndo mpigaji au hata akikupigia ni simu za kukuomba vocha baada ya tafadhali niongezee salio kutokufanya kazi....
Msichana michezo ya kukuchezea akili hua anaanza kipindi unamtongoza, ile ya kukujaribu kama kweli umemfia na unampenda kuliko waleti yako ila akiwa na uhusiano hata mara moja huwa haendi njia hii. Hii kijana sina shida ya kukufafanulia sana maana mtendwa ni wewe, ukishaona hichi mlango wa kutoswa u mbeleyako na hata kama hujatoswa bado nahisi ni vocha zako tu ndo zinazokuweka mjini.
  • Anachelewa kupokea simu zako....
Unajaribu kumpigia mara kadhaa simu inaita tuu..., na sio mara moja ni kitendo kinachoendelea siku baada ya siku, hata akipokea anakua amesha poteza hali ya upendo na wewe, muongeaji unakua wewe, yeye kazi ni kuitikia tu..!, ule mchangamko aliokua anao zamani hana tena, zile simu za saa tatu usiku muda wa chombeza zinakua hazina mvuto tena, mazungumzo mwanzoni yalikua hayaishi kila kitu kinanoga inaweza fika usiku wa manane nyie ndo kwanza  mnajua ni saa nne na nusu usiku, sasa hivi hata dakika ishirini zikiisha ni tizi, kaka jiongeze!.
  • Anapoteza hamu ya kufanya mapenzi na wewe....
Sasa hivi zile ahadi za wikiendi tena ndo zimekwisha tena, hata kama zipo ni kidogo sana kutokea, romance hazina mzuka tena kama awali, anakua kama anatimiza wajibu tu kutokana na vihela vyako unavyompatia na vocha, ila zile hisia huzioni, sio kwamba wewe unaishiwa nguvu za kiume ila mazingira na mapokeo ndo yanamfanya mzee mzima awe na jaziba akasirike kupita kiasi au alegee na kuruzi interesti!.
  • Hafuatilii tena maswala yako...
Zile shida zako mlizokua mnatatua pamoja sasa ni wewe pekee yako, yeye ukimgusa lazima akuambie yupo bize na kitu flani, sidhanii hii inaitaji digrii ya sayansi kuelewa nini kinaendelea kati yenu, Hata kama ni shida ya kifedha sasa hivi imebezi upande mmoja tu, na siku zote kama ndo umependa lazima ufate amri, japo roho inauma naunajua kabisa mazingira ya mapenzi yenu yalipofikia ni pabaya ila unajipa moyo kama hauoni, kaka kama umeshindwa kurekebisha ufa, ni heli uachie nyumba ianguke ujenge upya.
  • Utambulisho wa marafiki wake tena hamna...
Sasa hivi utambulisho kwa marafiki zake hamna tena maana kwa sasa mambo mengi anayofanya utakua ushilikiswi, hata ukishilikishwa lazima itatokea sababu atakayoifanya yeye itakayokufanya wewe usihudhurie, na hata ikitokea ukiwa wewe na baadhi ya marafiki zake, utambulisho utarukwa, kwa kupindishwa na stori zingine ambazo hazihusiani kabisa.

SOMA ALAMA ZA NYAKATI,
Kiumeni.com tunachokuambia lazima usome alama za nyakati na uchukue tahadhari kabla mambo hayajaharibika, ili kuweza labda kufanya juhudi za kurudisha mambo yawe kama zamani na kumrudishia hamasa zake au ule mvuto wa mapenzi aliokuanao awali, au kama yameharibika sana usikutwe na mtoso bila wewe kuujua umetokea wapi na kukukuacha moyo umepasuka ukashindwa kufanya hata shughuri za kujenga taifa na maisha yako kwa ujumla, ni rahisi kudili na mtoso unao uona unakuja kuliko ule unaotokea ghafla.

COMMENTS

Jobstanzania
Name

Fasheni,3,Jua Zaidi,10,Mahusiano,19,Mazoezi,4,Mchezaji wa Mapenzi,22,Picha Maneno,14,Slider,6,Top Stories,12,WaulizeWanaume,3,
ltr
item
Kiumeni - WaulizeWanaume.: Ukiona Hivyo ujue Moyo Wake Na Hisia Zake Za Mapenzi Zimepungua Juu Yako Na Hana Furaha Tena Na Wewe Na Bado Kidogo Ataondoka.
Ukiona Hivyo ujue Moyo Wake Na Hisia Zake Za Mapenzi Zimepungua Juu Yako Na Hana Furaha Tena Na Wewe Na Bado Kidogo Ataondoka.
Utake usitake jambo halitokei bila dalili, hata mvua haitokei ikanyesha tu bila mawingu kuonekana. Hata kama sie mwanaume mwingine ndo anamchanganya ila dalili hizi zinaonyesha inawezekana mwisho wa uhusiano ndo kitu kikubwa kinachofatia, na wala usiwaze ndoa.
http://3.bp.blogspot.com/-kK3V5PYsHWU/U48thIxjcRI/AAAAAAAAAmY/_F11Vk9XSgo/s1600/unhappy-couple-in-bed-pf.jpg
http://3.bp.blogspot.com/-kK3V5PYsHWU/U48thIxjcRI/AAAAAAAAAmY/_F11Vk9XSgo/s72-c/unhappy-couple-in-bed-pf.jpg
Kiumeni - WaulizeWanaume.
http://www.kiumeni.com/2013/07/ukiona-hivyo-ujue-moyo-wake-ushahamia_29.html
http://www.kiumeni.com/
http://www.kiumeni.com/
http://www.kiumeni.com/2013/07/ukiona-hivyo-ujue-moyo-wake-ushahamia_29.html
true
5715942833127633596
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy