Jinsi Ya Kutongoza Ni Ngumu, Ila Kwa Mjuzi Wa Kutongoza Hufuata Njia Hizi...

Kila mtu anauwezo wa kumtongoza msichana tatizo lazima ujue nini unafanya, kipi kinatakiwa kutangulia na kipi kinatakiwa kufuatia, kumtokea msichana ni jambo ambalo limekuwa gumu kwa watu wengi, mtu anaweza kumpenda msichana na inawezekana anaishi nae karibu tu na kila siku anaonana nae ila hafanyi chochote!.

''Mjuzi wa kutongoza ni mtanashati, mtaalam wa kutongoza ni msafi na tofauti na unavyofikiri, mara nyingi mjuzi wa kutongoza sio sharobaro na wala sio kwamba anamistari mikali saana, sema ni mcheshi na anajua kusifia pale panapohitajiwa kusifiwa na anajua kuongea pale neno linapotakiwa kuongelewa!''
Kila mtu anauwezo wa kumtongoza msichana tatizo lazima ujue nini unafanya, kipi kinatakiwa kutangulia na kipi kinatakiwa kufuatia, kumtokea msichana ni jambo ambalo limekuwa gumu kwa watu wengi, mtu anaweza kumpenda msichana na inawezekana anaishi nae karibu tu na kila siku anaonana nae ila hafanyi chochote!.Wanawake hawapendi wanaume hambao hawana maamuzi, kuwa na maamuzi, jikakamue na onyesha hisia zako, penye nia pana njia. Tatizo wanaume wengi wanaogopa kutoswa tena hamna anaeongoza kutoswa kama mkufunzi wa mapenzi, ila tatizo la mkufunzi wa mapenzi anajifunza kutokana na makosa, kumbuka hata wewe darasa la pili kipindi kile hesabu za kujumlisha ulikua unakosa, ila sasa hivi hesabu ya 1+1 unaiona ya kitoto sababu ulijifunza kutokana na makosa uliokua unafanya. Unaanza na uwanafunzi kwanza ndo unaenda kwenye ualimu.

Kiumeni.com tunakunyambulia vitu unavyotakiwa kuvijua ukitaka kuwa mtu unaejua mchezo wa kutongoza. Nifuatilie vizuri, na hakikisha unafanya majaribio na utaona mabadiliko. Na ukitoswa usivunjike moyo ndo mwanzo na hata hivyo kisicho riziki hakiliki, hii ni hesabu ya kujumlisha, kuwa na moyo utaijua tu!.
  • NAMBA MOJA; KUJIAMINI... 
Unatakiwa uwe unajiamini, hamna kitu ambacho hawa viumbe wenye jinsia tofauti na sisi wanachokijua zaidi kukiona kama kumuona mwanaume ambae hajiamini, na ndio sababu kubwa ya kutoswa, kutojiamini. Maana mwanaume asie jiamini mwanamke atampeleka wapi... mwanamke anahitaji baba wa familia!, sasa yeye na wewe mtu usiojiamini wapi na wapi!, maana kwa vyovyote atakuona kuwa hauna maamuzi madhubuti, na yeye anataka mtu wa kumuongoza, kwahio ukimfata hakikisha upo unajiamini na aone unajiamini.
  • NAMBA MBILI; PANGA SWAGA ZAKO USIKURUPUKE....
Msichana hafatwi moja kwa moja, ukitaka kuharibu pozi na kumfata kichwa kichwa utachoambulia ni ''Unikome, tena usinizoee kaka...'', kuwa mtulivu soma mazingira kama simba muwindaji. Panga swaga zako, mwangalie machoni kwa mbali akigeuka akakuona unamwangalia tabasamu kidogo endelea na mambo yako huku unamtupia jicho mara kwa mara, usiogope wala usionyeshe hujiamini kila mtu na mtu wake kwa jinsi ulivyo na wewe una uzuri wako hambao hujioni.
Siku zote ukienda kichwa kichwa pozi la kufanya mazungumzo yaendelee hua linaisha haraka sana, utajikuta umetupa maneno mawili matatu, la nne huna la kusema!, mtoto kumbe anaendelea kukusikiliza wewe betri imeisha!, unamkosa kijinga tu!, hakikisha umemsoma toka mbali na cha muhimu zaidi angalia lugha yake ya mwili kama yupo na wewe, alipokushitukia unamwangalia mapokeo yake yalikuaje?, maana kama kaanza kuuma kucha toka mbali, au kuangalia chini anakuonea aibu au ulipotabasamu nae katabasamu, jua kaka hio ni mali yako..!, cha kufanya sogea karibu na usaini mkataba!. Kumuangalia toka mbali na kumsoma ni vizuri tena sana, maana unaweza kuta mtoto yuko kwenye mudi mbaya, wewe ukapata gia ya kumuingia kwa kumpa pole na kumpoza!, sasa kama hajamchunguza toka mbali si unaweza kuta unamchekea kumbe mtu anamajonzi au hasira ukaishia MATUSI!. Kwa hio kumsoma kwa mbali na kumtupia jicho moja mbili... mpaka yeye akagundua unamwangalia nakutabasamu inatayarisha mazingira zaidi nakuyafanya yawe murua na ukiona anakurudishia jicho kali mpotezee utamtafuta siku nyingine akiwa vizuri zaidi.
Ukitaka mambo yaende vizuri zaidi usiwe na haraka, chukua muda wako onyesha unamtaka kihisia, unaweza hata kumpa siku kadhaa huku unamwonyesha unavyopendezwa nae, hii inampa muda na yeye akuone wewe ni mtu wa namna gani, wasichana wanapenda sana mtu mwenye subira na inamfanya msichana akuzoee hata kabla hamjaaanza kuongea na pia ina mto hofu kuhusu wewe na inakupa manufaa ya kutengeneza mazingira ya maongezi yawe ya kelewana na kueleweka zaidi.
  • NAMBA TANO; UNAKAZI ZA KUFANYA....
Msichana anampenda mtu wa maendeleo, mtu anaethamini kazi na mtu aliebize na shughuri zake, kwa hio usikosee ukafanya akuone kama mtu mzembe usie na kazi ya kufanya, itakushushia heshima na usijue kipi ulichovuruga. Kuwa bize na mambo yako ila ukimwona mwonyeshe kwa macho na tabasamu kuwa yupo akilini mwako, sio siku nzima unamzinga kama mwizi unataka umtaimu umuibie.

Kwa hiyo umempata huyu msichana ambae unataka umtongoze uongee nae, umeshamwangalia jinsi lugha yake ya mwili ilivyo, unacheza nae kwa macho na tabasamu nae anamapokeo mazuri tu na kuna ka asilimia kadogo kwamba anaweza kukataa na hujali hilo kwa sababu kwa prea kutoswa kutakua ni sehemu ya mchezo, ukitoswa usichukulie moyoni sana ni sehemu ya kujifunza ili ukirudi ujue wapi ulikosea.

COMMENTS

Jobstanzania
Name

Fasheni,3,Jua Zaidi,10,Mahusiano,19,Mazoezi,4,Mchezaji wa Mapenzi,22,Picha Maneno,14,Slider,6,Top Stories,12,WaulizeWanaume,3,
ltr
item
Kiumeni - WaulizeWanaume.: Jinsi Ya Kutongoza Ni Ngumu, Ila Kwa Mjuzi Wa Kutongoza Hufuata Njia Hizi...
Jinsi Ya Kutongoza Ni Ngumu, Ila Kwa Mjuzi Wa Kutongoza Hufuata Njia Hizi...
Kila mtu anauwezo wa kumtongoza msichana tatizo lazima ujue nini unafanya, kipi kinatakiwa kutangulia na kipi kinatakiwa kufuatia, kumtokea msichana ni jambo ambalo limekuwa gumu kwa watu wengi, mtu anaweza kumpenda msichana na inawezekana anaishi nae karibu tu na kila siku anaonana nae ila hafanyi chochote!.
http://1.bp.blogspot.com/-ZV1NP1XyVpw/VWwg3z5p7lI/AAAAAAAAAzw/bupBu0kjAwk/s640/Kutongoza%2B-%2B-kiumeni.com.jpg
http://1.bp.blogspot.com/-ZV1NP1XyVpw/VWwg3z5p7lI/AAAAAAAAAzw/bupBu0kjAwk/s72-c/Kutongoza%2B-%2B-kiumeni.com.jpg
Kiumeni - WaulizeWanaume.
http://www.kiumeni.com/2013/08/kutongoza-ni-ngumu-ila-kwa-prea-hufata_1.html
http://www.kiumeni.com/
http://www.kiumeni.com/
http://www.kiumeni.com/2013/08/kutongoza-ni-ngumu-ila-kwa-prea-hufata_1.html
true
5715942833127633596
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy