Sifa wanawake wanazopenda, wanazoangalia na kuzitafuta kwa mwanauwe...

Kuna sifa nyingine wanawake wanaziangalia kwa mwanaume ambazo hazihusiani kabisa na muonekano, hizi sifa ni za muhimu sana maana zinamtambulisha mwanaume jinsi alivyo kwa undani. WaulizeWanaume wameweza kukuandalia sifa zinazokuza hamasa kwa mwanamke, na sababu kwanini kila mwanaume anatakiwa azizingatie na kuzionyesha kwa yule anayemfanya moyo wake uende mbio...

"Kila mwanamke hupendezwa nazo, hufikiria na kusari ili mwanaume atakae kuwa nae au ambae anaye awe nazo!."
 Kila mwanamke ana orodha ya vitu anavyovipendelea kwa mwenza wake, inawezekana ikawa urefu, rangi ya ngozi au chochote kingine, mara nyingine haiwezekani kujibadilisha ili kuendana na sifa wapenzi wetu wanazopendelea.
Kuna sifa nyingine wanawake wanaziangalia kwa mwanaume ambazo hazihusiani kabisa na muonekano, hizi sifa ni za muhimu sana maana zinamtambulisha mwanaume jinsi alivyo kwa undani.
kiumeni.com wameweza kukuandalia sifa zinazokuza hamasa kwa mwanamke, na sababu kwanini kila mwanaume anatakiwa azizingatie na kuzionyesha kwa yule anayemfanya moyo wake uende mbio...

            1: Awe mwenye shauku na kujari...

Kuwa na shauku na mpenzi wako na kuonyesha jinsi gani unavyo mjari na anavyo kuvutia na sio tu kimapenzi pekee bali na kihisia pia, kuwa na shauku kwenye vitu vinavyo mpendezesha kuanzia kikazi mpaka kwenye maisha yake kijamii, mwanamke anapenda sana mwanaume anayejua kujari na kumpa msaada pale anapouhitaji.

            2: Awe anaejiamini...

Kujiamini ni jambo moja ambalo ni muhimu sana kwa mwanamke, na huliangalia kwa macho yote mawili kuanzia wakati unapomtongoza, maana wanawake wanapenda wanaume wanaojiamini na wanaojua nini hasa wanafanya na wanataka katika maisha yao, hii sifa wanaitumia ili kumpata mwenzi anaejiamini na anayeweza kuwa baba wa familia, hii sio kuhusu tu kwa jinsi unavyo fanya vitu kwa watu wengine bali kwa muuonekano wako kiujumla kwa jamii.

           3: Awe mwaminifu...

Wanawake hawapendi mtu ambaye ni muongo, hawapendi kudanganywa na kama ni kitu ilihaidi kufanya basi na ufanye katika muda ambao umeuhaidi kufanya, zaidi ya hapo wanapenda utulivu wako kwa wasichana wengine, hawapendi mwanaume ambae ni kiruka njia, ambae hawezi kutulia kwenye uhusiano na msichana mmoja, wanawake wakiingia kwenye uhusiano, huwa wanaingia ili wakae kwa muda mrefu na wanapenda wenzi wao wawe hivyo vivyo.

           4: Awe msiri na asiyeeleweka...

Wanawake wanapenda kusisimka, hasa kwenye mahusiano mapya, na hakuna njia nzuri ya kufanya msisimko uendelee kwenye mahusiano kama kwa kuwa msiri, fanya usiri mzuri kwa kumshitukiza mpenzi wako kwa zawadi au jambo ulilolifanya kwa siri, hii huongeza hamasa ndani ya mapenzi na katika uhusiano.

             5: Awe mkarimu...

Wanawake wanapenda ukarimu na ni moja ya vitu wanavyoviomba sana kwa mungu wapenzi wao wawenavyo, kuwa mkarimu kwa yeye na watu wote wakuzungukao, hii ni sifa wanawake wakikijua unayo na upo singo lazima wakukimbilie tofauti na wanaume wanaofikiria kuwa mwanaume anapaswa kuwa mgumu, kwa wanawake hili ni tofauti.

            6: Awe anayejua kutumia maneno...

Wanawake wanapenda kufurahi na wanapenda mwanaume anayefanya wakae na furaha na vicheko, unatakiwa kutumia maneno vizuri kumfanya mpenzi wako ajisikie vizuri kuwa nawe, na hata kama amekasirika, kununa au yupo kwenye majonzi tafuta maneno ambayo yatamfanya arudishe tabasamu lake.
Hizo ni sifa sita ambazo kila mwanamke hutamani mweza wake awe nazo, na ukizitumia vizuri hakika hakuna mwanamke atakaye baduka pambeni yako na siku zote atakutamani mpaka mwisho wa maisha yake.

COMMENTS

Jobstanzania
Name

Fasheni,3,Jua Zaidi,10,Mahusiano,19,Mazoezi,4,Mchezaji wa Mapenzi,22,Picha Maneno,14,Slider,6,Top Stories,12,WaulizeWanaume,3,
ltr
item
Kiumeni - WaulizeWanaume.: Sifa wanawake wanazopenda, wanazoangalia na kuzitafuta kwa mwanauwe...
Sifa wanawake wanazopenda, wanazoangalia na kuzitafuta kwa mwanauwe...
Kuna sifa nyingine wanawake wanaziangalia kwa mwanaume ambazo hazihusiani kabisa na muonekano, hizi sifa ni za muhimu sana maana zinamtambulisha mwanaume jinsi alivyo kwa undani. WaulizeWanaume wameweza kukuandalia sifa zinazokuza hamasa kwa mwanamke, na sababu kwanini kila mwanaume anatakiwa azizingatie na kuzionyesha kwa yule anayemfanya moyo wake uende mbio...
http://3.bp.blogspot.com/-SNcIOvOMYuY/UyQI0lK3gLI/AAAAAAAAAQU/1Q6-4kBiw2M/s1600/black-couple-in-bed.jpg
http://3.bp.blogspot.com/-SNcIOvOMYuY/UyQI0lK3gLI/AAAAAAAAAQU/1Q6-4kBiw2M/s72-c/black-couple-in-bed.jpg
Kiumeni - WaulizeWanaume.
http://www.kiumeni.com/2014/03/sifa-wanawake-wanazoangalia-na.html
http://www.kiumeni.com/
http://www.kiumeni.com/
http://www.kiumeni.com/2014/03/sifa-wanawake-wanazoangalia-na.html
true
5715942833127633596
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy