Unaujua mvuto wa kimapenzi na siri zake, unajua ni nini kinachomfanya mwanamke avutike kwako na alama za iwapo kama atakukubali ukimtongoza?

Mwanamke ameumbwa kutoka kwenye ubavu wa mwanaume na siku zote mvuto wa mwanamke au hamasa juu ya mwanaume uwa ipo kwa kipindi chote ila kinachotofautisha hali ya upendo ya mwanamke kuvutika na wewe au la, ni kiasi cha mvuto[hamasa] alichonacho juu yako.

"Mwanamke ameumbwa kutoka kwenye ubavu wa mwanaume na siku zote mvuto wa mwanamke au hamasa juu ya mwanaume uwa ipo kwa kipindi chote ila kinachotofautisha hali ya upendo ya mwanamke kuvutika na wewe au la, ni kiasi cha mvuto[hamasa] alichonacho juu yako."

Najua hujanipata vizuri hapo, kaa vizuri sasa ili uweze kunielewa hii mada tunayoiongelea siku ya leo ndani ya kiumeni.com, naona hapa tungetumia mfano ingekuwa vizuri zaidi.

Kwa mfano; Abeli amevutika na Aneti na ndo amemuona kwa siku ya kwanza huyu msichana wa kipare aliye mzuri kwa urembo wake usio na kifani, kabla Abeli hajamuendea Aneti kumsemesha, mvuto wa kihisia wa Aneti tukichukulia kwa asilimia 1 mpaka 100 unakua asilimia 40%, hii inatokana na sababu ya kuwa siku zote kibaiolojia mwanamke huvutika kwa mwanaume.

Iwapo mwanamke atakua na asilimia 100% ya mvuto kwako huyu hata kuwa na haja wala hata sababu ya wewe kumtongoza maana tayari atakua ameshavutika na upendo juu yako tayari umeshawaka moto, atakuwa anajipendekeza na kujigonga kwako kwa hali ya juu, hata ukimwambia aende kuiba benki akeletee kila kitu atafanya kwa uaminifu mkubwa.

Akiwa na hamasa ya asilimia 0%, hapa hata ukimzawadia kisiwa cha malavidavi na kumfanya awe malkia wa nchi ili kuwa na wewe haitowezekana na hata akiwa na wewe inakua kwa sababu ya kimasirahi tu.

Akiwa na hamasa ya kati ya asilimia 51% kwenda juu hapo kunauwezekano wa kumbadilisha maamuzi na kufanya kuundwa kwa uhusiano wa kimapenzi na kimahaba ila unahitajiwa kuwa mbunifu na mwanaume kiongozi.

Ili uongeze mvuto na kumfanya mwanamke ahamasike na wewe inatokana na sababu ndogondogo utakazo kuwa nazo na zile utakazozisababisha kwa kipindi hicho ambacho unamuona na kuongea nae na kuufanya mvuto wake kwako upungue au uongezeke, ili mwanamke aonyeshe kupenezwa na wewe inabidi awe na hamasa ya asilimia 51% au juu ya hapo.

Iwapo mwanamke akikuona kwa mara ya kwanza na akapendezwa na muonekano wako na kwa macho yake akakuona ni mtanashati mwenye sura nzuri, basi hapo hamasa yake inakuwa ipo asilimia 70%, ila akikuona umependeza kawaida hapo hamasa yake[mvuto wake] ipo katikati asilimia 50%.

Mwanaume anayekuwa na mvuto kwa mwanamke kwa asilimia 50% ambaye anazijua changamoto na jinsi ya kuwa muungwana na mwanaume kiongozi anaweza kuipandisha hio hamasa ya mwanamke ya asilimia 50% ikaenda juu zaidi, unaweza kuanza kwa kuwa na hamasa kubwa kwa mwanamke ila ikashuka chini zaidi na hapo itakuwia ngumu kumpata maana mvuto wake kwako utakua umepungua pamoja na kuwa na sura nzuri ya kitanashati, na yule aliyeanza na mvuto mdogo akaweza kuipandisha na mwisho wa siku yeye ndo akawa kinara na kuondoka na mtoto.

Kwa mwanaume ambaye mvuto wa mwanamke anaetaka kumtongoza upo chini ya asilimia 45% inabidi awe mbunifu na kama umepiganae hadithi nzuri na ukamfanya acheke na kutabasamu na mwisho wa maongezi mkabadilishana namba za simu basi tumia nafasi yako vizuri pale mnapoacha inakubidi uwahi kumpigia simu ili asije akakusahau na uendelee kupandisha hamasa yake kwako.

Vitu vinavyo ongeza mvuto wa hisia za awali alizonazo mwanamke kufikia kiwango cha kumfanya haamasike kihisia na wewe, ni vitu viwili vikuu kama kiumeni.com inavyokunyambulishia ifuatavyo,
 • #1, Muonekano wako na utanashati wako;
Sio kwamba kuwa na sura nzuri ndo kutakufanya kila mwanamke avutike na wewe, ila inaongeza kiasi cha mvuto kwa mwanamke kwake, na hii itampa faida zaidi maana mvuto atakaoanza nao wa mwanamke utakuwa wa juu wa asilimia 70% na hii kutamfanya asihangaike sana wakati wa utongozaji, hii haimaanishi ya kuwa hawezi kukataliwa maana muonekano si kitu kikubwa cha kipekee kinachoangaliwa kwenye mvuto wa mwanamke.
 • #2, Jinsi ulivyojitambulisha na maongezi uliyoyaongea;
Kujiamini na kuweza kumfanya mwanamke atabasamu na kufurahia kile unachozungumza na uwepo wako kwa ujumla ndo jambo kuu linaloweza kukufungulia nafasi kubwa ya kukubaliwa kimapenzi, matamanio ndani ya ubongo wa mwanaume yameelekezwa machoni wakati matamanio katika ubongo wa kike yameelekezwa masikioni, ndo maana kumraghai mwanamke ni vyepesi zaidi kuliko kumraghai mwanaume na hupandisha kiwango cha mvuto wa mwanamke kwa hali ya juu sana.

"Zingatia kitu kimoja, mwanamke akivutika na wewe atakuonyesha ishara nyingi za kukusaidia ili umtongoze, hapa ikiwemo kukuangalia kwa macho mazuri, kuongea nawe katika hali nzuri na ya kuvutia huku akicheka na kutabasamu".

 Kuna alama za kuangalia na kujua kipimo cha mvuto[hamasa] kwa mwanamke kabla ya kumtongoza kama kiumeni.com inavyozidi kukuelezea, haya maelezo yananifanya nimkumbuke mjomba wangu anavyosema "Akipendezwa na wewe, atakusaidia kwa kukuonyesha njia ya kumtongoza kwa kukupa ishara".

Ishara nzuri mwanamke anazotoa hamasa ikiwa asilimia 50% kwenda juu;
 • Ukimtabasamia nae anakutabasamia,
 • Anaangalia chini halafu pembeni,
 • Anatoa ishara za mapokeo (anapikicha nywele, kama amevaa jaketi anafungua vishikizo, anaiachia mikono yote huru, anajisogeza karibu).
 • Anapindisha kichwa kidogo,
 • Anaongeza kiasi cha kufumba na kufumbua kope za macho,
 • Ukiongea nae anakuonyesha hali ya kimaongezi.
Ishara mbaya mwanamke anazozitoa hamasa ikiwa chini ya asilimia 40% kushuka chini,
 • Anaangalia pembeni kwa haraka,
 • Hapindishi wala kukichezesha kichwa chake,
 • Hana ishara za mapokeo (anakunja mikono kifuani),
 • Ukiongea naye anakujibu kwa mkato.

COMMENTS

Jobstanzania
Name

Fasheni,3,Jua Zaidi,10,Mahusiano,19,Mazoezi,4,Mchezaji wa Mapenzi,22,Picha Maneno,14,Slider,6,Top Stories,12,WaulizeWanaume,3,
ltr
item
Kiumeni - WaulizeWanaume.: Unaujua mvuto wa kimapenzi na siri zake, unajua ni nini kinachomfanya mwanamke avutike kwako na alama za iwapo kama atakukubali ukimtongoza?
Unaujua mvuto wa kimapenzi na siri zake, unajua ni nini kinachomfanya mwanamke avutike kwako na alama za iwapo kama atakukubali ukimtongoza?
Mwanamke ameumbwa kutoka kwenye ubavu wa mwanaume na siku zote mvuto wa mwanamke au hamasa juu ya mwanaume uwa ipo kwa kipindi chote ila kinachotofautisha hali ya upendo ya mwanamke kuvutika na wewe au la, ni kiasi cha mvuto[hamasa] alichonacho juu yako.
http://4.bp.blogspot.com/-xCHUTyQy_lQ/U5DJtvsz5RI/AAAAAAAAAms/LTQ8qhLUVvo/s1600/mvuto-www.waulizewanaume.com.jpg
http://4.bp.blogspot.com/-xCHUTyQy_lQ/U5DJtvsz5RI/AAAAAAAAAms/LTQ8qhLUVvo/s72-c/mvuto-www.waulizewanaume.com.jpg
Kiumeni - WaulizeWanaume.
http://www.kiumeni.com/2014/06/unaujua-mvuto-wa-kimapenzi-na-siri-zake.html
http://www.kiumeni.com/
http://www.kiumeni.com/
http://www.kiumeni.com/2014/06/unaujua-mvuto-wa-kimapenzi-na-siri-zake.html
true
5715942833127633596
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy