Baada ya maneno matamu na vicheko, unaanza kumtongoza....

"Oooh, mie nina rafiki wa kiume, moyo wangu umeisha jaa tayari, maana ninae nimpendae.. labda tuwe marafiki tu, umechelewa!". P...

"Oooh, mie nina rafiki wa kiume, moyo wangu umeisha jaa tayari, maana ninae nimpendae.. labda tuwe marafiki tu, umechelewa!".
Paa.. kidume moyo unakudunda, akili inasizi, uwezo wa kufikiria unakuwa hafifu' huna hili wala lile, na kama ndo hivyo upendo ulikuwa umeisha kuchukua, taratibu mwili unalegea, miguu inaanza kukosa nguvu maana netiweki ya ubongo haifanyi kazi tena, unatamani kutamka mstari mtamu wa kimapenzi ili umlainishe mtoto, unakosa cha kuongea.., kama vile umeusahau, unabaki kupigwa na bumbuwazi!, ilishawahi kukutokea hii?.

Hili hapa ndo tukio kama linavyoweza kutokea; tuseme upo sehemu, kidume ukekaa umetulia tuli!, kwa mbali mara unamuona mtoto mzuri, kwa urembo alionao anakufanya akili na macho yako yastaajabu na tabasamu lako taratibu linajiachia kwa kumkubali jinsi alivyo, kama zali mtoto nae anakutabasamia, huku jicho lake la husuda likiwa na wewe, kwa lugha yake ya kimwili na jinsi na yeye anavyokuangalia unajipa moyo mtoto yupo kwenye mazingira ya kutongozeka.

Isiwe shida! moyoni unawaza, unaamua kuinuka kwa mapozi yako ya kutosha uyajuayo wewe, unamkaribia na kuanza kujitambulisha na maongezi yanakwenda vizuri kwa vicheko vya hapa na pale, mpaka pale anapokupasulia bomu machoni...

"Oooh, mie tayari nina rafiki wa kiume, moyo wangu umeisha jaa tayari, maana ninae nimpendae.. labda tuwe marafiki tu, umechelewa!".

Mstari mbaya sana huu ambao kiukweli unakufunga kazi zote za ubongo na kushindwa kufikilia vizuri, mtego wa panya ambao huwa hauna pa kutokea.

Mara nyingi huwa ni mstari wa kujiahami ambao mwanamke huutumia ili kukupunguza kasi hasa unapokuwa na haraka sana ya kumtongoza maana anakuwa hakujui we ni nani, upoje, tabia yako hususani ni ya aina gani maana inawezekana ukawa ni jambazi usiku, na asilimia 80% ya wanaume wanaoambiwa hivi huwa ndio kwa mara ya kwanza ndo wanakutana na huyo mwanamke au ndo mara ya kwanza kuongea nae.

Sio kila mwanamke ni sawa, wanawake ni tofauti na hutofautiana kwa uwezo wa uelewa na kisaikolojia, hii hutokana na jinsi mwanamke alivyokuzwa na mambo mbali mbali yaliomtokea kwenye maisha, hivyo hivyo na wakati wa utongozaji iwapo ukikariri utongozaji wa aina moja utajikuta unakumbwa sana na haya mambo maana jinsi mwanamke mmoja anavyoamini na kumkubali mtu kwa wepesi ni tofauti kabisa na mwanamke mwingine anavyoweza kufanya hivyo.

Kama kawaida kiumeni.com hukuambia na itazidi kukuambia, pole pole ndio mwendo na simba mwenda pole ndio mla nyama, usiwe na haraka ya kusema yale yaliyo moyoni mwako, cha kwanza na cha kuangalia mpe muda wa mwanamke akufahamu, akuzoee na kukujua wewe ni mtu wa aina gani, haimaanishi mara uonapo mwanamke kapendezwa na kupenda kampani yako kwa maongezi ndo hapo hapo uanze kumtongoza, msome na mjue ni aina gani ya mwanamke, ikiwa hauna uhakika mwambie umependa maongezi yake na ungependa kuendelea na hayo maongezi siku nyingine hivyo akupe mawasiliano ni kwa jinsi gani utampata, subira huvuta heri na atakuona wewe ni aina tofauti ya mwanaume maana umependa kumjua kwanza na hauna haraka naye hivyo hata akikutana nawe haupo kwa kumtamani pekee.

Iwapo umemtogoza mwanamke na amekuambia anaye ampendaye na sio kuwa ndo kwa mara ya kwanza ndo mnazungumza ama kuonana hapo kidogo ni shida, kitu cha kwanza huwa ni cha kwanza, haimaanishi amekuingia moyoni kiasi gani, umemtamani kiasi gani au unamarengo nae kiasi gani, kitu kimoja cha kufanya ni kumsahau na kumtoa akilini kabisa huyu msichana, maana hii humaanisha msichana hajakupenda au hajaona iwapo mnaweza kweli mkaendana, na wala usije puuzia ukaona labda anakupima kukuona ni kwa kiasi gani unaweza kumsumbukia, huu msitari mwanamke akiutumia humaanisha hayuko tayari kuanzisha uhusiano na wewe.

Kama mwanamke kapendezwa na wewe, hukusaidia kukupa njia za kumtongoza, kama ni kimaongezi atajiweka kimaongezi zaidi, kama yupo kwenye kundi la watu atajisogeza pembeni ili apate kuzungumza na we kwa uzuri zaidi, ila akionyesha dalili tofauti na hapo kwa kukupa majibu ya mkato na kukuambia anaye ampendae basi hapo umekutana na jiwe lisilopasuka na kama ni bahati yako sio hapo ilipo.
 Na kunauwezekana akawa anakuambia hivyo sababu kwa muda huo anachohitaji ni rafiki wa kawaida pekee, inawezekana alikuwa kwenye uhusiano wa muda mrefuu, ameachana na wewe ndo ukaona nafasi na fursa imejitokeza ya wewe kuwa nae, kama kuwa nae kama rafiki utaweza japo utahitaji subira, unaweza kusubiri na kuwa nae kama rafiki labda mambo yanaweza kubadilika kadri ya miezi inavyozidi kwenda na siku moja subira yako ikazaa jambo siku za mbeleni, kama tu utakuwa mtaratibu na mwenye subira kubwa.

Inaweza kutokea akaja kukutambulisha pia kwa marafiki zake wa kike ukawa haujapoteza sana, tofauti na hapo kuwa mtaratibu na mtakie siku njema na endelea na mambo yako.

Jua, fahamu, elewa na kuwa mwanaume bora zaidi, www.kiumeni.com.

COMMENTS

Jobstanzania
Name

Fasheni,3,Jua Zaidi,10,Mahusiano,19,Mazoezi,4,Mchezaji wa Mapenzi,22,Picha Maneno,14,Slider,6,Top Stories,12,WaulizeWanaume,3,
ltr
item
Kiumeni - WaulizeWanaume.: Baada ya maneno matamu na vicheko, unaanza kumtongoza....
Baada ya maneno matamu na vicheko, unaanza kumtongoza....
http://3.bp.blogspot.com/-6o9gEthsCd8/VP10TPO51RI/AAAAAAAAAHY/NkR2AgGDSCg/s1600/www.kiumeni.com.jpg
http://3.bp.blogspot.com/-6o9gEthsCd8/VP10TPO51RI/AAAAAAAAAHY/NkR2AgGDSCg/s72-c/www.kiumeni.com.jpg
Kiumeni - WaulizeWanaume.
http://www.kiumeni.com/2015/03/baada-ya-maneno-matamu-na-vicheko.html
http://www.kiumeni.com/
http://www.kiumeni.com/
http://www.kiumeni.com/2015/03/baada-ya-maneno-matamu-na-vicheko.html
true
5715942833127633596
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy