Jinsi Ya Kumfanya Msichana Unayemtongoza au Uliyenaye Kwenye Mwanzo wa Uhusiano Awe na Hisia na Akupende Kupitiliza.

Kumfanya msichana ahamishe akili kwako au japo kumfanya apendezwe na wewe huwa ni ngumu, ila kumfanya msichana akupende na achanganyikiwe kupitiliza juu yako?, hili hua ni mlima kilimanjaro wa ugumu wa changamoto za kimahaba japo kuwa inawezekanika na thamani yake inakuwa kubwa zaidi.

Kumfanya msichana ahamishe akili kwako au japo kumfanya apendezwe na wewe huwa ni ngumu, ila kumfanya msichana akupende na achanganyikiwe kupitiliza juu yako?, hili hua ni mlima kilimanjaro wa ugumu wa changamoto za kimahaba japo kuwa inawezekanika na thamani yake inakuwa kubwa zaidi.

Kweli unataka kumvutia huyo msichana spesho aliyeuteka moyo wako na kukufanya usile usilale kwa mawazo juu yake achanganyikiwe na kukuweka wewe akilini mwake endelea kusoma kiumeni.com tukuweke wazi ni nini na ni kipi ufanye uuteke moyo wa huyo mrembo kwa marefu na mapana, na awe anakuwaza wewe tu na kukufikiria wewe kokote anako kwenda.

Kiumeni.com, nyumbani kwa wanaume tunakupa njia za kufanya ambazo zinahitaji utulivu, subila na kuzielewa kwa kina ili uweze kufanikisha wakati wa kumtongoza au mwanzo wa mahusiano ili huyu mrembo akuweke moyoni na rohoni.

      #1; Kuwa shujaa wake...

Wakati wote anapokuwa na shida, matatizo au amekumbwa na mawazo yanayomtinga na kumchanganya akili, hakikisha unakuwa naye pamoja, na si kwa kukaa pembeni yake tu bali kwa kuonyesha dhahiri umeguswa na upo nae bega kwa bega kutafuta utatuzi, ufafanuzi wa kumwondolea dhahama iliyopo mrangoni kwake, weka jambo moja kichwani na unisikie vizuri, sio kila jambo utaliweza kulitatua na hicho pia akimaanishi kwa kuwa jambo lipo nje ya uwezo wako ndo hautakuwa na msaada, hata ushauri na maneno ya kumpa moyo yanatosha kumfanya uwe shujaa katika dunia yake hasa katika wakati wa matatizo.

Muulize ni kwa jinsi gani unaweza kumsaidia ila usiwe king'ang'anizi wa kutoa msaada wakati bado moyo wake haujakubaliana na wewe katika msaada huo, usitumie razima, tumia maneno mazuri ambayo ataona upo kwa ajiri ya kumsaidia na si vinginevyo.

Kama tayari ameshaonyesha kupendezwa na wewe, nenda nje ya mipaka yako na fanya kitu ambacho kitamstaajabisha na kama bado hajaonyesha kupendezwa na wewe, tumia utaratibu, subira na upole na atajikuta kaingia kwenye kumi na nane mwenyewe, kama wahenga wasemavyo "maneno mazuri humtoa nyoka pangoni".

    #2; Hakikisha asikuchukulie kama rafiki...

Fanya urafiki naye ila siyo kila saa unakaanaye karibu sana naye, heshima hushuka hasa mtu mkizoeana sana na kwa mwanamke hupoteza ile hali ya mvuto na hamasa na kuanza kukuona mtu wa kawaida, na iwapo akikuchukulia kama rafiki au kaka, kumrudishia tena hisia ili akuchukulie zaidi ya hapo huwa inakuwa ni ngumu.

Hakikisha kwa muda wote unapokuwa nae mwonyeshe kwa kumjari kuwa unahisia nae, na sio kwa kumwambia ila acha vitendo vyako vyenyewe vizungumze juu ya kile moyo wako unachojisikia na atakuona wewe ni mwanaume wa kipekee maana vitendo kwa mwanamke hukonga moyo zaidi tofauti na maneno hewa na ahadi zisizokwisha, na hii itampa urahisi mwanamke kujua ni kundi gani ndani ya moyo wake atakalokuweka, akuweke kihisia au kirafiki.

  #3; Mpe muda wa kukuwazia upo wapi na unafanya nini...

Siyo kila saa ni saa ya kuongea naye au kuwa naye, ukisha muweka karibu na kunfanyia vitendo vya wazi ni kipi kilichomo moyoni mwako ni vizuri ukawa unampa muda wa kuwa naye mbali ili naye akufikirie, kuongeza mvuto na kujua uzito wako kwenye maisha yake kwa ujumla, afikirie vitendo vizuri unavyomfanyia, kwa jinsi atakavyokuwa anaendelea kukuwaza ndo jinsi ambavyo nawe unamwingia akilini na kuuteka moyo wake.

Najua unajua ila ningependa nikujulishe zaidi, kama wahenga wasemavyo "mtu akikuzoea sana, dharau huanza na anakua anakuchukulia kwa wepesi", kwa hio mazoea ni mabaya hasa mwanzo mwa uhusiano au kipindi cha utongozaji, na hapa kaka sijaongelea mazoea yale ya kawaida ya kumfanya aondoe uwoga juu yako, naongelea mazoea ya kupitiliza ya kumafata fata mwanamke kama kuku.

 
  #4; Angalia na tilia mkazo unachovaa...

Marafiki wa kawaida hawawezi kujali iwapo umerudia nguo zile zile ulizokuwa umezivaa tangia jana ila msichana wa ndoto zako huwezi kumuingia akilini iwapo ukiwa katika hali ya uchafu na kutokuwa nadhifu, kwa utafiti uliofanyika katika chuo kimoja jijini washingtoni marekani cha saikolojia na tabia za binadamu , unadhifu huwavutia zaidi ndo maana kisaikolojia wanawake wanapokutana na mtu kwa mara ya kwanza humuangalia juu mpaka chini, inawezekana ukajua wakati anakutathimini au usijue ila ni jambo ambalo lazima mwanamke hulifanya, na kwa kufanya hivyo huweza kukutambua tabia zako na jinsi unavyoishi na iwapo ukiongea nae, huweza pia kutambua tabia ya hisia yako kama wewe ni mkali au mpole na tabia nyinginezo.

Kama kaka angu Abeli asemavyo, "uvaaji wa binadamu na jinsi anavyokaa kimwili ni dirisha la roho yake, maana humuongelea yote na jinsi maisha yake yalivyo".

Hakikisha unaoga na kuwa msafi na nadhifu, kama unandevu zinyoe ziwe katika stairi na hali nzuri, nukia kuwa nadhifu na vaa nguo zinazoendana na mwili wako, fanya mazoezi ya mara kwa mara kuufanya mwili wako kuwa katika hali ya kiume na kishupavu na inayovutia zaidi.

  #5; Kuwa mcheshi...

Unatakiwa uwe jampo kidogo mcheshi, ucheshi unamfanya mwanamke akuzoee mapema kwa muda mfupi na kumfanya ajiamini akiwa pembeni yako, kuwa mtu mwenye urahisi kimaongezi, mfanye atabasamu akiwa pembeni yako na afurahie kile kitendo cha yeye kuwa karibu yako mkifurahi pamoja na kubadilishana hadithi za kimaisha za hapa na pale, mfanyie vitu vya kumjali na kumfurahisha kwa vitendo na maneno matamu na muonyeshe yeye ndie wa pekee anayeumiliki moyo na nafsi yako.

Kuwa na uelewa wa kiakili, jua nini cha kuzungumza kulingana na mazingira, jua mambo mbalimbali ya kijamii ili upate wigo mkubwa wa kuzungumzia na kamwe usionyeshe hata kidogo hali ya ujuwaji wa uwewe ndie wewe... kila kitu ndo unakijua.

    #6; Kuwa mtu wa uhakika na kuaminika...

Wanawake hupenda mtu wa uhakika, tenda kutokana na kile ulichomuhaidi na kuongea na kama ulitoa ahadi, vitendo ulivyovihaidi vifanye katika muda uliopanga kuvifanya, usiwe mzungushaji wa mambo, na iwapo ukiahidi kufika sehemu hakikisha unalinda muda ulioupanga utafika, wanawake hawapendi kumsubilia mtu, wanahisi kama umeshindwa kumthamini na kumchukulia katika uzito unaotakiwa, kama vile unamchukulia juu juu na hivyo nafsi yake itabadilia na kuanza kukuchukulia na wewe juu juu.

Na katu usitumie utani kwenye mapenzi, utani utani uliovuka mpaka hukutoa katika ngazi ya juu ya moyo wake na kukuweka kama mtu wa kawaida, utani uondoa uhakika, ukimwambia kitu atakuwa anahisi unamtania.

Utani ndo nguzo kubwa itakayokufanya akutoe moyoni na kukuona kama rafiki.

Kuwa na sifa nzuri mtaani ili hata kama yeye au rafiki zake wakikufanyia uchunguzi wakuone wewe ni wa uhakika na siyo wakute sifa chafu ambazo zitakuondolea sifa nzuri unazoumia na kutumia nguvu kubwa kuzijenga, sifa kama ulimwacha mpenzi wako wa zamani kwa ajiri ya msichana mwingine ndo hasa zitakazokuondoa moyoni mwake na atakuchukulia kama muongo fulani ambae kwake hautafuti kingine bali kile kilichopo ndani ya chupi yake.

Jiheshimu na onyesha heshima kwa unavyompenda na sio kutumia maneno machafu ya aibu ya kihuni na hapo kwake moyoni utamuingia kwa sababu anauhakika na kukuamini wewe.

   #7; Usiwe king'ang'anizi wa mambo...

Hakuna kitu kinachompunguzia sifa mwanamke kama saa zote upo naye, saa zote upo mkiani kwake, akikata huku upo, akigeuka hivi anakutana na wewe, inawezekana bado hata hajakuweka wazi kama amependezwa na wewe au la, mpe nafasi mtoto wa watu, mpe muda wa kutokuona na fanya vitu vya kuvutia kwake na hapo ndipo ataona thamani yako, mtengenezee hali ya kukosa uwepo wako na hicho ndicho kitu kitakachomfanya awe na hamasa kubwa sana na wewe.

Msichana akikuambia hataki jambo fulani liache, maana kama halitaki hataki kweli na kumg'ang'aniza ni kumboa maisha yake na ataanza kukuona wewe ndie dosari iliyopo kwenye maisha yake, na akiona hivyo tu jua ndio kwaheri mwalimu, steringi ndo anafia hapo.

Kumlazimisha msichana hata kama unamlazimishia jambo zuri ni kuuwa hisia zake kwako, wanawake hupendwa kubembelezwa na kutumia maneno mazuri, maneno mazuri humtoa nyoka pangoni, na hii haimaanishi siku hio hio ndo nyoka atatoka kuwa na uvumilivu na tumia ubunifu.

   #8; Kuwa na uwezo wa kujitegemea...

Wanawake huwa hawajari ni shilingi ngapo ulizonazo mfukoni, najua... najua unachowaza, sizungumzii wale milupo na wapenda pesa, nazungumzia mtoto aliyefundwa kwao na baba na mama yake vizuri, wanachoangalia ni uwezo wako wa kumkidhia mahitaji yake, upendo unagharama ili unoge, mtatulie shida ndogo ndogo zake, mjari na kumfanya afurahi, hii inamaanisha kuna ka gharama kadogo ka kumnunulia asali ili mapenzi yakolee, kuwa na kazi na kuwa na uchumi wako binafsi ambao utakusaidia kutatua mambo madogo madogo ili uweke fikra kichwani mwake za kutamani kuolewa na wewe maana unauwezo wa kumtimizia mahitaji yake na unampenda vilivyo.

Kumjali ndo kitu pekee kitakachompa mawazo juu yako na utamtengenezea hali ya kukukosa moyoni iwapo utakuwa mbali naye, utamtengenezea fikra za kukuwaza sababu unampenda na kumjali.

   #9; Usionyeshe kuvutika na kupendezwa na wasichana wengine...

Msichana akianza kukupenda wewe ujue wivu nao ni sehemu ya mapenzi, jieshimu na yeye atakuthamini kwa kukupenda sababu anajua moyoni hana sababu ya kuwa na wasi wasi maana wewe ni wake na upo kwa ajili ya kazi moja, kumpenda mpaka matiti yake yaanguke, kumpenda mpaka nywele zake zibadilike rangi kuwa nyeupe, kumpenda mpaka ngozi yake ikunjamane.

Tumia heshima na muonyeshe unampenda yeye pekee na sio kuchungulia chungulia wasichana wengine kila anapokutazama, muonyeshe mungu kamtengeneza yeye pekee kutokea kwenye ubavu wake na hamna msichana anayeweza kukufurahisha kama anavyofanya yeye, tabasamu lake ni tosha kupoteza neno kinywani ambalo ulilotaka kuliongea.

  #10; Msifie na mjurishe kwa maneno matamu unavutiwa naye...

Hakuna msichana ambae hapendwi kusifiwa, kumsifia kunaongeza kujiamini kwa msichana na kukupa wewe uhuru zaidi wa kumuonyesha unavutika naye hivyo kumuongezea hamasa zaidi juu yako, tumia maneno matamu na malaini kumsifia na kumwonyesha yeye ni spesho.

Mwanzo wa mahusiano hautakiwi kutumia sifa zinazomlenga maumbo yake ya mwili maana ataona ndio ulichokifuata kwake, usitumie sifa kama...

  • Umefungashia uko nyuma mpaka unataka kunifanya nisiamini kile nacho kiona.
  • Lips zako zinangaa na pana kiasi natamani kukuondoa lipstiki kwa ulimi.
  • Matiti yako bolibo mamaa, napoyaona moyo unanienda mbio.
Sifa hizi humfanya msichana mwanzo wa uhusiano akuone hauna mapenzi ya kweli na awezi kukuweka moyoni sababu hana sababu ya kufanya hivyo, zaidi ataona unamzingua tu.

Tumia sifa nzuri kama kumsifia juu ya...

  • Sauti yake
  • Jinsi alivyopendeza siku hio na awe amependeza kweli na sio kutoa sifa ovyo ovyo.
  • Jinsi uelewa wake ulivyo mpana na ungependa kumsikiliza saa zote.
  • Uzuri na urembo wake kwa ujumla bila kugusia kiungo chochote cha mwili.
  • Na mengine mengi unayoyaona yanahaki ya kusifiwa.
Usitoe sifa kila mara maana utaondoa uzito wa sifa yenyewe na kukuona kila wakati wewe ni wa kumsifia tu, kwa vyovyote atana kama unafanya mzaha, angalia na seheme ya kutoa hio sifa, kama kiumeni.com tusemavyo, mazingira yakiwa mazuri, sifa ndio inasifika zaidi na kumuacha mtoto wa watu na tabasamu na tamaa ya kuendelea kukusikiliza.

Ukiona stori zimenoga hapo ndio sehemu nzuri ya kumuagia na kuondoka zako, itasababisha awe anakuwaza na kutamani kuongea nawe zaidi na taratibu unaanza kumchukua moyo wake.

Ili umuingie moyoni, jiamini na kuwa wewe kama wewe, jaribu kujenga mahusiano kwa jinsi mahusiano yeyewe yanavyoelekea, kuwa mbunifu jiongeze na jua lengo lako ni kutaka kumfanya kila akigeuza shingo, fikra yake kichwani iwe inakuwaza wewe, jua, fahamu elewa na kuwa mwanaume bora zaidi, www.kiumeni.com

COMMENTS

Jobstanzania
Name

Fasheni,3,Jua Zaidi,10,Mahusiano,19,Mazoezi,4,Mchezaji wa Mapenzi,22,Picha Maneno,14,Slider,6,Top Stories,12,WaulizeWanaume,3,
ltr
item
Kiumeni - WaulizeWanaume.: Jinsi Ya Kumfanya Msichana Unayemtongoza au Uliyenaye Kwenye Mwanzo wa Uhusiano Awe na Hisia na Akupende Kupitiliza.
Jinsi Ya Kumfanya Msichana Unayemtongoza au Uliyenaye Kwenye Mwanzo wa Uhusiano Awe na Hisia na Akupende Kupitiliza.
Kumfanya msichana ahamishe akili kwako au japo kumfanya apendezwe na wewe huwa ni ngumu, ila kumfanya msichana akupende na achanganyikiwe kupitiliza juu yako?, hili hua ni mlima kilimanjaro wa ugumu wa changamoto za kimahaba japo kuwa inawezekanika na thamani yake inakuwa kubwa zaidi.
http://3.bp.blogspot.com/-S_f78-84zjQ/VPWPEwsuAKI/AAAAAAAAAGw/Oj_HBcKtO60/s1600/blackwomanthinking.jpg
http://3.bp.blogspot.com/-S_f78-84zjQ/VPWPEwsuAKI/AAAAAAAAAGw/Oj_HBcKtO60/s72-c/blackwomanthinking.jpg
Kiumeni - WaulizeWanaume.
http://www.kiumeni.com/2015/03/jinsi-ya-kumfanya-msichana_4.html
http://www.kiumeni.com/
http://www.kiumeni.com/
http://www.kiumeni.com/2015/03/jinsi-ya-kumfanya-msichana_4.html
true
5715942833127633596
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy