Ishara, Mapozi na Lugha ya mwili ya mwanamke ndo nguzo kuu ya mafanikio ya utongozaji.

Amini usiamini, wanawake hutoa ishara kila mda ya nini wanafikilia, wanajisikia na nini wanachokihitaji kwa muda husika,ishara hizi huonek...

Amini usiamini, wanawake hutoa ishara kila mda ya nini wanafikilia, wanajisikia na nini wanachokihitaji kwa muda husika,ishara hizi huonekana wazi kwa jinsi ambavyo miili yao inavyokaa na kubadilisha pozi.


Watu wengi hufikiri wakati wa utongozi mwanaume ndio mchaguzi wa uwanzishaji wa kumtaka mwanamke, kama ni msomaji wa kiumeni.com hili jambo tumeshawahi kuligusia, kwa utongozaji wowote uliokamilika kwa mafanikio mwanamke ndo huwa anaanzisha kumtongoza mwanaume bila kusema neno hata moja.

Kwa maneno mengine mwanamke huanzisha na kumsababisha mwanaume anzishe kumtongoza kwa kutumia lugha ya mwili wake kumuashilia mwanaume kuwa yupo katika hali ya mapokeo ya utongozwaji, na hivyo ndivyo ilivyo vijana, na umeisikia hapa kwanza kiumeni.com.

Mzoefu wa utongozaji ambae anaujua mchezo huu vizuri, mafanikio yake huwa hayapo kwa pamba alizopiga au muonekano wake mkali alionao, ila ni kwa sababu ni muongeaji mzuri anaejiamini na kujua kuisoma lugha ya mwili ya mwanamke aliokaa katika hali nzuri kwa kutongozwa.

Kwa kusoma lugha ya mwili ya mwanamke, nauwezo wa kumgundua mwanamke katika baa ambaye labda hana furaha na mwanaume aliekaa nae karibu, anaetamani kuburudika na haja zake za kimwili au anaetamani tu kuongea katika hali ya maongezi mazuri na matamu.

Usihangaike na kutaka kujua anafikiria nini, soma lugha yake ya mwili.
Waheshimiwa wengi wanachokosea huwa ni kutokujua umuhimu wa lugha ya mwili badala yake wanajaribu kuwa makini kutaka kujua nini kinachoendelea kwenye akili ya mwanamke, wanasimama kwa masaa mengi na vinywaji mkonono wakijiuliza kama mwanamke amependezwa nae au vipi. kidogo wakijuacho kuwa jibu lipo wazi iwapo tu wangekuwa wanamsoma mwanamke kwa mapozi yake na lugha yake ya mwili.

Usijichoshe kwa kutaka kumsoma na kumjua ni nini kinaendelea akilini mwake, hata Mwenyezi Mungu mwenyewe hushangazwa na kinachoendelea kwenye kichwa kigumu kueleweka cha mwanamke, Achana na hayo jaribu tu kuangalia lugha ya mwili wake na pozi anazozitumia maana zitakuambia yote unayohitaji kuyajua, na nikikuambia kusoma lugha ya mwili hapa sizungumzii na sijazungumzia ndo uwanze kuangalia matiti yake, hapa nazungumzia lugha ya mwili kwenye mapozi yake na macho yake zinazokuashilia anatamani kuongea nawe, anapendezwa na jinsi maongezi kati yenu yanavyo kolea kwa uzuri na utamu.

Kwa bahati mbaya mara nyingi wanaume kwa jinsi tulivyo na akili zetuzinazoshindwa kufikilia vizuri mbele ya hawa viumbe wazuri na wakupendeza watupagawishao akili, huwa tunajisahau kuangalia lugha za kimwili na pozi wanawake wanazotufanyia au huwa tunashindwa kuzielewa hizi ishara ambazo wanawake hutufanyia kupitia mapozi ya kimwili. ila weka kumbukumbu juu ya hili - kila kitu kuhusu mazungumzo na mwingiliano wa kimaongezi hutegemeana na sababu mbili zifuatazo:

Kwanza, mawasiliano huwa ni asilimia 60% ishara, pili ishara huwa na nguvu mara tano zaidi ya maongezi yanavyoweza kumaanisha, kwa hio kama hujaweka fikra zako kwenye ishara, mapozi na lugha yake ya kimwili unakosa asilimia 60% ya mchezo mzima unaoendelea kati yako na yeye, halafu mwisho wa siku unabaki unajiuliza kwanini mara zote ukirundi nyumbani upo peke yako mwishoni mwa usiku.


Jifunze jinsi ya kusoma ishara, mapozi na lugha ya mwili ya mwanamke na mwisho wa usiku iwe ni wewe na yeye nyumbani kwenye utulivu wa shuka baridi za kitanda chako.

COMMENTS

Jobstanzania
Name

Fasheni,3,Jua Zaidi,10,Mahusiano,19,Mazoezi,4,Mchezaji wa Mapenzi,22,Picha Maneno,14,Slider,6,Top Stories,12,WaulizeWanaume,3,
ltr
item
Kiumeni - WaulizeWanaume.: Ishara, Mapozi na Lugha ya mwili ya mwanamke ndo nguzo kuu ya mafanikio ya utongozaji.
Ishara, Mapozi na Lugha ya mwili ya mwanamke ndo nguzo kuu ya mafanikio ya utongozaji.
http://1.bp.blogspot.com/-pIdTnFNpSSE/VVnouFx2EkI/AAAAAAAAAus/kbaR07h9wJY/s640/flirting-woman-h-4.jpg
http://1.bp.blogspot.com/-pIdTnFNpSSE/VVnouFx2EkI/AAAAAAAAAus/kbaR07h9wJY/s72-c/flirting-woman-h-4.jpg
Kiumeni - WaulizeWanaume.
http://www.kiumeni.com/2015/05/ishara-mapozi-na-lugha-ya-mwili-ya.html
http://www.kiumeni.com/
http://www.kiumeni.com/
http://www.kiumeni.com/2015/05/ishara-mapozi-na-lugha-ya-mwili-ya.html
true
5715942833127633596
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy