Mshangaze Msichana Wako Apendezwe Nawe zaidi. Iwe ndio Unamtongoza au upo naye kwenye Mahusiano kupitia Rafiki Zake.

Ufunguo wa moyo wa mwanamke huwa ni kupitia kwa rafiki zake, kama rafiki zake wakipendezwa na wewe, huyo mwanamke aliekukonga moyo basi nawe utakuwa umeanza kuuteka taratibu, kiufupi utakuwa umeupata kila kitu kuhusu yeye, namba ya mwenye nyumba wake mpaka namba ya jirani yake, ukiwafurahisha rafiki zake basi bara bara yako ya wewe na yeye imeshaanza kuwa nyeupe.

Ufunguo wa moyo wa mwanamke huwa ni kupitia kwa rafiki zake, kama rafiki zake wakipendezwa na wewe, huyo mwanamke aliekukonga moyo basi nawe utakuwa umeanza kuuteka taratibu, kiufupi utakuwa umeupata kila kitu kuhusu yeye, namba ya mwenye nyumba wake mpaka namba ya jirani yake, ukiwafurahisha rafiki zake basi bara bara yako ya wewe na yeye imeshaanza kuwa nyeupe.

Hakuna kitu kinachomjulisha mwanamke unayemtongoza au uliye nae kuwa umetumwa na Mungu kuwa mpenzi wake kama kukuona wewe ukiwa unapatana na marafiki zake. Marafiki wa karibu wa mwanamke ndio majaji wanaokujaji kuwa ukoje, unatabia gani na kama unafaa kweli kuwa kipenzi cha rafiki yao mpenzi, maana wao ndio wanaomshauri na wao ndio nguvu ya umaa ya kimawazo kwenye kichwa cha huyo msichana umpendae.

Ila kuna sanaa ambayo kiumeni.com leo hii inataka kukufahamisha, kukujuza na kukuelekeza, sanaa ambayo ni nyepesi kueleweka na wala usiwe na shaka.

Kuwa unajua iwapo ukiparamia mti na kwenda kwa papara lazima zikutokee puani kwa mawili. Ukienda kwa kujifanya wewe ndio unaojua kutengeneza urafiki na kuwa rafiki kupitiliza lazima wakushitukie na kuondoa shauku yako kwako kwa kukuona ni mfuatiliaji tu wa kupotezea mda au mzushi flani unayewachimba kwa sababu ya rafiki yao, na pia iwapo ukienda kwa ukimya utaonekana kauzu, unaojidai na kuwaona wao sio lolote sio chochote na iwapo wakikuendekeza utamfanya rafiki yao wanao mjua tokea kitambo kabla ya wewe kuonyesha sura yakoajitenge na wao.

Nachojaribu kukufahamisha unatakiwa uwe kama maji, usiwe ya moto na usiwe ya baridi, na kiumeni.com itakusaidia kukupa maelezo ya kina ya jinsi ya kuwaingia.

1. Waulize majina yao. Kumbuka majina yao na ukiwa unayatumia usiyatumie kuwaita kwa ufupi, fanya hivyo iwapo watu wote wengine wanafanya hivyo pia.

2. Waulize maswali kuhusu wao. Uliza maswali mengi hata kama mengine yanaboa, kama kuna jambo ambalo wanataka kulifanya kwa pamoja jifanye kabisa kama unataka kulijua kwa marefu na mapana, na hakikisha ukiwa unauliza jambo hilo kuwa kama ndo umevutiwa na jambo kuliko ambavyo umeweza kuvutiwa na kitu chochote katika maisha yako.

3. Waambie jinsi ambavyo rafiki yao kipenzi anavyokuvutia na kukuchanganya. Hakikisha lugha unayoitumia sio kwa kuwalingishia kuwa huyu rafiki yao ndo mzuri kupita wao, tafuta rugha nzuri nyepesi maana unaongea na wanawake vile vile, kwa rugha isiwe kana kwamba unawaringanisha. Jua jambo moja kwa yote utakayoyaongea hapo yatakuwa kichwa cha habari baada ya wewe kuondoka, watakuongelea na kuyapima maneno yako kwa kina.

Muongelee rafiki yao kama ni mtu uliependezwa nae na amekushika rohoni, waambie kuwa jinsi unayoendelea kumjua rafiki yao ndivyo unavyoendelea kumpenda zaidi.

4. Wasifie. Ila hakikisha unakuwa na mpaka, wasifie kuhusu nguo zao, kazi zao au radha yao kwenye vitu flani flani walivyonavyo, hakikisha sifa zako zisiongelee miili yao au nyuso zao, iwapo ukifanya hivyo ujue watakuhukumu kama mtu unaevutika na kila mwanamke anaekatisha kwenye macho yako, na juu ya yote unaanza kuonyesha hisia za kuwatongoza mbele ya rafiki yao.

5. Kama upo umetoka nao kwenye mtoko, wanunulie vinywaji na kama anaishi na marafiki zake, njoo na chupa ya waini ya dompo au saint anna siku nyingine ukija, hii inamaanisha utakuwa umejitengenezea picha nzuri na kuonekana mtu muungwana, mwenye roho nzuri, usio na choyo na unamapenzi ya kweli na rafiki yao.

Kuwafanya rafiki wa mpenzi wako uliyenae au mtarajiwa wakupende na kitu kimoja ambacho kitakupa sifa nzuri sana, maana hata kama msichana hajapendezwa sana na wewe harafu marafiki wamekupenda ujue utatetewa vizuri na uhakika wa kuwa na huyo msichana umpendae utakuwa mkubwa, na kitu kimoja kuhusu wanawake, wanawake wanategemea sana ushauri kutoka kwa marafiki zao, hivyo hata kama ukiwa umekosea jambo na upo kwenye uhusiano na huyo msichana umpendae, ukiwa upo poa na marafiki zake ujue utakuwa na watetezi wa kufanya msamaha wako uwe nje nje kupitishwa.

COMMENTS

Jobstanzania
Name

Fasheni,3,Jua Zaidi,10,Mahusiano,19,Mazoezi,4,Mchezaji wa Mapenzi,22,Picha Maneno,14,Slider,6,Top Stories,12,WaulizeWanaume,3,
ltr
item
Kiumeni - WaulizeWanaume.: Mshangaze Msichana Wako Apendezwe Nawe zaidi. Iwe ndio Unamtongoza au upo naye kwenye Mahusiano kupitia Rafiki Zake.
Mshangaze Msichana Wako Apendezwe Nawe zaidi. Iwe ndio Unamtongoza au upo naye kwenye Mahusiano kupitia Rafiki Zake.
Ufunguo wa moyo wa mwanamke huwa ni kupitia kwa rafiki zake, kama rafiki zake wakipendezwa na wewe, huyo mwanamke aliekukonga moyo basi nawe utakuwa umeanza kuuteka taratibu, kiufupi utakuwa umeupata kila kitu kuhusu yeye, namba ya mwenye nyumba wake mpaka namba ya jirani yake, ukiwafurahisha rafiki zake basi bara bara yako ya wewe na yeye imeshaanza kuwa nyeupe.
http://2.bp.blogspot.com/-fHVprTDw2dc/VXBk2q3SC3I/AAAAAAAAA1E/MRL__C-qYUI/s640/Marafiki%2Bzake%2Bwa%2Bkike%2B-%2Bkiumeni.com.jpg
http://2.bp.blogspot.com/-fHVprTDw2dc/VXBk2q3SC3I/AAAAAAAAA1E/MRL__C-qYUI/s72-c/Marafiki%2Bzake%2Bwa%2Bkike%2B-%2Bkiumeni.com.jpg
Kiumeni - WaulizeWanaume.
http://www.kiumeni.com/2015/06/mshangaze-msichana-wako-apendezwe-nawe.html
http://www.kiumeni.com/
http://www.kiumeni.com/
http://www.kiumeni.com/2015/06/mshangaze-msichana-wako-apendezwe-nawe.html
true
5715942833127633596
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy