Njia 10 za kumfanya mwanamke akufukuzie na kukutaka baada ya kumuonyesha hisia.

Zifahamu njia 10 zinazo weza kumfanya mwanamke akufukuzie na kukutaka baada ya kumuonyesha hisia zako. Ukizifahamu na kuzielewa njia hizi 10 basi utakuwa mkufunzi wa kiumeni na kuwafanya watoto wenyewe wa kike wawe wanakuhangaikia.

Huwa tunatumia mda mwingi sana hapa kiumeni tukiongelea, sehemu gani nzuri ya kukutana na wanawake, jinsi ya kuwatongoza na kuanzisha maongezi, nini cha kuongea na kufanya ili akuelewe na mrembo awe wako, na kadhalika.. Lakini hayo yote ambayo huwa tunayaongelea huwa ni kama theruji kwenye mlima kilimanjaro, ila volukano yenyewe huwa ni jinsi ya kuwafanya wanawake waanze kukuhangaikia na kukufuatilia, na hizi hapa ni njia kumi za kuwa mkufunzi wa kiumeni na kuwafanya watoto wenyewe wa kike wawe wanakuhangaikia.Naomba nitilie mkazo jambo moja, njia hizi hakikisha hauzichukulii juu juu, zielewe na zitunze vizuri kwenye akili yako, maana unahitaji kila kitu uwe umeshakielewa kwa yote tuliozungumzia hapa kiumeni kuhusu wanawake.

Namba 1. Tengeneza mvuto unaovutia kwake mara ya kwanza unaongea nae.

Kitu kimoja wanaume wengi wanacho kiharibu na kupoteza nafasi yeyote ya kuwafanya mwanawake aanze kumfuatilia kwa kuharibu mambo tokea mwanzoni, ni pale mwanaume unapopata nafasi na kuanza 'aaahaa' na 'eeehee, si unajua.. aahaa', na kuonyesha tabia ya kutojiamini na kuwa na wasiwasi, tabia ambayo humfanya mwanamke asivutike tena na wewe, ukimuuliza mwanamke yeyote ni kitu gani anachovutiwa kwa mwanaume, cha kwanza atakuambia anapenda mwanaume anayejiamini.

Sifa ya mwanaume wa kweli huwa ni kujiamini, na mwanamke sikuzote anavutika na mwanaume wa kweli, onyesha kujiamini na kuwa mkufunzi wa mchezo wa kutongoza toka moyoni bila hata kufikilia utaongea nini au kujishitukia, utaona mwanamke mwenyewe hata kama angekuwa amekutegea mgongo atageuka na kuanza kukusikiliza kwa mvuto, mkibadilishana namba kesho mwenyewe ndo atapiga simu na kuanza kujitambulisha, "Halo, mie ndo yule dada tuliobadilishana namba", mwenyewe anaanza kujinogesha, kukufatilia na kukuwinda.

Namba 2. Muonyeshe changamoto.

Hili kiumeni tumeshaliongelea, mwanamke akihisi wakati unamtongoza kuwa umeshakufa kwake ukaoza, huna mwingine yeye ndio yeye, unamuhitaji kupitiliza kwa hiyo utafanya chochote, moja kwa moja anakuweka kwenye kundi la FALA, (Samahani kwa kutumia kiswahili kibaya, ila ndo hivyo), mwanamke sikuzote huwa havutiki na mwanaume Fala, mwanaume ambaye mapenzi yanamuendesha hana la kufanya zaidi ya kumlamba miguu, kama waswahili wasemavyo "Ukimwonyesha mwanamke unampenda sana, lazima atakusumbua", wanawake hawavutiki na mwanaume fala, mwanaume ambae anaweza kumpelekesha jinsi yeye anavyotaka, sasa atawezaje kukufatilia wakati havutiki na aina hio ya wanaume, tofauti na hapo anajua tu lazima mwenyewe utajipeleka.

Tokea binadamu kuumbwa, mwanamke huwa anapenda kitu ambacho hawezi kukipata, na hata kama akikipata na akajua kakipata lazima hamu ya kuwa nacho imwishie na kukitaka kingine ambacho hana uwezo nacho, ndivyo fikra na akili ya mwanamke ilivyo, umenielewa hapo jamaa?

Onyesha changamoto, mwonyeshe hutawaliwi na tamaa na huendeshwi na mapenzi, unamambo mengi ya kufanya, na kama una marafiki wa kike hakikisha anawajua, ili ajue kumpenda yeye ni uamuzi na sio lazima maana wapo wengi, muonyeshe wewe ni kati ya wale wanaume wachache kupatikana, mwanaume lijali ambaye wanawake wote wameumbwa kutoka kwenye ubavu wake mmoja tu kati ya mbavu nyingi alizonazo. Hivi haujawahi kuona mwanamke anampenda sana mwanaume halafu mwanaume hana hisia na huyo msichana, unajua msichana huwa anakuwaje?

Namba 3. Muulize maswali ya namna flani.

Mwanamke akishakusoma na kukuona wewe ni mwanaume wa aina flani, kuna uhakika mkubwa ataendelea kukufikilia kuwa wewe ni mwanaume wa aina hiyo, kwa hivyo ukianza kuonyesha tokea mwanzo we ni mwanaume yule anaye lilia mapenzi, basi ataanza kukuona fala tokea mwanzo, mwanaume ambae utamfuata fuata hata pale ambapo hautakiwi, na unajua wanawake wanahisia gani na wanaume wa aina hii. Kwahio ukianza na maswali ya kuonyesha tabia ya kifala, patishia.. huyo mwanamke ataanza kukufikilia kuwa utakuwa na tabia hizo hizo kwa kipindi chote cha maisha yako, na huwo ndo utakuwa mwisho wako.

Kwahiyo ni vizuri ukaondoa kabisa maswali ya kuonyesha kama wewe ni mtu ambaye hujiamini, maswali kama "Kwa hio ni aina gani ya wanaume unaowapenda?", au "Vipi, hivi mie naendana na wewe?" baya zaidi ni "Hivi unamvulana?" Hivi unauliza anamvulana ili iweje, kama umevutika naye fanya yako kwanza, uhusiano ukiwa umejenga muhimili mwenyewe atajua sheria zinasemaje, tafadhali usijaribu maswali ya namna hii.

Namba 4. Usimfatilie sana.

Usipoonana na mtu sana mara kwa mara hukufanya uanze kumkumbuka, na hii kanuni ukiitumia vizuri kwa mwanamke utamfanya aanze kukuulizia kwa rafiki zako, iwapo ungeitumia hata kwa naniii hata hizo meseji ambazo hakujibu angekuwa anazijibu. Iwapo ukiwa unapendelea kumuona ona huyo mwanamke, au husubili na kumpa muda mwanamke kumpigia simu mara baada ya yeye kukupigia, utafanya siku zote uwe kwenye uhusiano wa upande mmoja, uhusiano wa wewe kuumia na mawazo na kujipendekeza kwake kwa kumramba miguu na kumfanya yeye asikujali. Iwapo akiwa anakutarajia kuwa utafanya hivi hapo kutakuwa tena hakuna kipaumbele kwa upande wake, hakuna ile hali ya kumfanya akufatilie wewe na kukutaka, tofauti na hapo kumfata fata kunampa maana nyingine mwanamke ambae ndo kwanza ameanza kupata hisia kwako, kunampa maana kuwa amekutana tena na Fala mwingine.

Ukimwonyesha tabia ya kumuhitaji sana lazima atakuona wa kawaida usio na uzito wowote kwake, ila ukijionyesha wewe ni kiumbe ambae haupatikani kirahisi, kiumbe wa nadra ambae akikukosa maishani mwake lazima atakuja kujutia nafasi, kutamfanya akutake na kuanza kukufatilia kwa ukaribu maana tayari anakuwa ameshagundua anakuhitaji wewe na wewe ndie yule mwanaume lijari aliyekuwa anamsubiria, maana upo tofauti na wanaume wengine anaowapuuzia.

Namba 5. Muonyeshe umempa akili yako na umakini kwa hali flani.

Habari ya Mjini: Wanawake wanapenda sana wakiwa wanaongea na mwanaume, na mwanaume huyo akawa anawapa umakini wa kuwasikiliza. Tofauti na hapo wanawake huwa wanaishiwa mvuto na mwanaume ambae anawapa umakini kiasi cha kupitiliza, umakini huu sio wa kusikiliza bali ule wa kuonyesha wewe ndo unaejua kupenda kwa kumpa sifa nyingi katika hali ambayo haziitajiki, kumnunulia zawadi bila sababu, kwa hio acha kumnunulia zawadi bila sababu na kumpa sifa pale ambapo haziitajiki, sio kwamba kidogo tu kabadili pozi, tayari na wewe umeshamsifia, kabla siku haijaisha tayari umeshamsifia mara 100. Mwisho wa siku atakuona unamsifia sifia tu kumshika masikio bila kumaanisha chochote kile ukiongeacho, na juu ya zawadi atakuona unampa mpa zawadi ili kununua upendo wake na wala hauna mapenzi yeyote ya dhati kwake.

Badala yake mwambie ulikuwa unamfikilia leo au mwambie umemuota jana, ili ajuwe yupo akilini mwako unamfikilia badala ya kumpa sifa mpaka azione za kawaida, unavyomsifia mara chache ndo husuda yake ya kutaka kusifiwa na wewe inavyokuwa kubwa, ndivyo atakavyokuwa na tamaa ya kusikia maneno kutoka kwako.

Namba 6. Mwingie kwenye kichwa chake.

Kumfanya mwanamke awe anakufukuzia, inakubidi umfanye mwanamke awe anakufikilia badala ya wewe kuwa ndie unayemfikilia, na njia moja ya kufanya jambo hilo lifanikiwe kwa urahisi ni: Kataa au zipuuzie mialiko au vitendo unavyovipokea tokea kwa mwanamke, ukitaka ufanikiwe kwa uzuri zaidi fanya uonekane upo bize na sio mtu wa kupatikana kwa wepesi. Mwambie, "Aah, unataka tutoke ijumaa hii? Sijui. Kuna ishu nyingine inatokea siku hio na sidhani kama huyu msichana ataniruhusu nisifike".

 Fanya hivyi kwa usahihi na hatoweza kukutoa akilini mwake.

Namba 7. Mringishie

Hii hatua ina umuhimu wake, kumfanya mwanamke aanze kukufatilia lazima ugeuze baadhi ya mambo, hii nikimaanisha lazima ujiweke wewe uwe kama mchaguzi, na mwanamke anatakiwa ajionyeshe kuwa anafaa kuwa na wewe.

Ila inabidi ufanye hii hatua kwa kuzingatia usije ukaonekana kama unajiona, tafuta staili ya kuifanya, fanya maongezi ya kirahisi kama kumuuliza "Hivi ni nini kinachokutofautisha wewe na wasichana wengine niliokwisha kuwa nao kimahusiano?" au "Ni vitu gani vitatu ambavyo unauhakika mwanaume atavipenda kwako, na tafadhari usiniambie uzuri", Muulize hivi ukiwa kama vile unafanya maongezi ya kutania na huyo mwanamke ataanza kuvutiwa na wewe kwenye maongezi, na hii haina uchawi.

Na pia unaweza kuwa umemwahidi kitu ambacho unajua anakipenda ila ukatumia pia kumcheleweshea kumpa, ukawa unamtamanisha kwa maneno mazuri, hali hii inaongeza mvuto zaidi wa kukitaka hicho kitu na kuongeza mvuto zaidi juu yako ila kuwa mwangalifu asigunduwe unamringishia.

Namba 8. Mfurahishe na Mchekeshe.

Kicheko ni kitu kilicho na nguvu sana kuuteka moyo wa msichana, na inabeba sababu ya kisayansi. Kumfanya mwanamke afurahie kuwa na wewe ni njia kuu ya kumfanya awe anafikiria kutumia muda wake na wewe na kukufikiria wewe pia.

Kwahiyo mfanye mwanamke achekelee na hata kama akiwa na msimamo kiasi gani, kibaiolojia atajikuta anavutika na wewe kwa sababu ya hisia nzuri anavyojisikia akiwa na wewe, hiyo hisia hawezi kuipuuzia zaidi ya kuendelea kukuwaza na kutaka kufahamu ulipo ili akufuatilie umpe tabasamu jingine.

Namba 9. Usionyeshe karata zako zote.

Hii njia ndio nayoipenda kupita njia zote ndani ya kiumeni.com kwa sababu ni njia rahisi na nzuri zaidi na inamfanya mwanamke afanye kazi zote, unachotakiwa kufanya ukikutana na mwanamke kwa siku ya kwanza usiwe kama redio, unatangaza matangazo yako yote, unaweza kuanza kufanya hivi kwa kutojitambulisha jina mpaka hapo atakapokuuliza jina lako, au kwa kumuwekea kichwani fikra ya "Labda." Mwambie "Sikia, natakiwa nirudi nikawape kampani rafiki zangu, labda ntaweza kukuona baadae."

Kwa njia hii kunamfanya asikutambue na akilini anabaki na labda, Labda ananitaka? labda kavutika nami? na siku zote mashaka na kutokujua ni njia moja nzuri sana ya kutengeneza mvuto. Ukimfanya apate zile hisia za kukutaka kukujua, zile hisia za mvuto wa kutaka kukufahamu, kutamfanya aanze kukufuatilia bila yeye kutokujua anafanya hivyo.

Namba 10. Acha kumfatilia.

Kama kila saa unashindwa kujizuia kumfatilia msichana, kutaka kujua anafanya nini, yupo wapi, kwa njia hiyo huwezi kufuzu kuwa na uwezo wa kumfanya msichana aanze kukufatilia wewe.

Kwa hiyo njia ya mwisho ni kuacha kumfatilia. Na hapo ndipo hiyo tabia ya kumfata fata mwanamke kama katoto kanyonyacho kinavyomlilia mama akiwa hayupo itakavyoisha. Utakuwa tofauti na wanaume wengine wanavyokuwa, wanawake watakuona mtu unaejiamini na kijua kile utakacho kutoka kwenye maisha yako mwenyewe na watavutika na wewe kwa mvuto wa mafanikio sio mvuto wa kupewa ahadi hewa. Anza kutengeneza tabia ambazo zinawavutia wanawake, tabia ambazo zitakuweka juu na kukufanya uwe kile mwanamke anachotamani kuwa nacho, tabia ambayo inampa mwanamke hamu ya kukutaka kukujua zaidi, kutaka kukufahamu, kutaka kukaa karibu yako, kutaka kukupa vitamu alivyonavyo ili mradi tu awe na wewe.

COMMENTS

Jobstanzania
Name

Fasheni,3,Jua Zaidi,10,Mahusiano,19,Mazoezi,4,Mchezaji wa Mapenzi,22,Picha Maneno,14,Slider,6,Top Stories,12,WaulizeWanaume,3,
ltr
item
Kiumeni - WaulizeWanaume.: Njia 10 za kumfanya mwanamke akufukuzie na kukutaka baada ya kumuonyesha hisia.
Njia 10 za kumfanya mwanamke akufukuzie na kukutaka baada ya kumuonyesha hisia.
Zifahamu njia 10 zinazo weza kumfanya mwanamke akufukuzie na kukutaka baada ya kumuonyesha hisia zako. Ukizifahamu na kuzielewa njia hizi 10 basi utakuwa mkufunzi wa kiumeni na kuwafanya watoto wenyewe wa kike wawe wanakuhangaikia.
https://2.bp.blogspot.com/-EciI7MfXhV8/VXWnViAG8hI/AAAAAAAAA18/DF4In7bsPMM/s640/Kufukuzia%2B-%2Bkiumeni.com.jpg
https://2.bp.blogspot.com/-EciI7MfXhV8/VXWnViAG8hI/AAAAAAAAA18/DF4In7bsPMM/s72-c/Kufukuzia%2B-%2Bkiumeni.com.jpg
Kiumeni - WaulizeWanaume.
http://www.kiumeni.com/2015/06/njia-10-za-kumfanya-mwanamke-akufukuzie.html
http://www.kiumeni.com/
http://www.kiumeni.com/
http://www.kiumeni.com/2015/06/njia-10-za-kumfanya-mwanamke-akufukuzie.html
true
5715942833127633596
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy